Zechariah 1:18-21

18Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! 19 aNikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?”

Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.”

20Kisha Bwana akanionyesha mafundi wanne. 21 bNikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?”

Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”
Copyright information for SwhKC